• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa sekta ya ujenzi wa miundo mbinu kati ya Rwanda na China wapata maendeleo mapya

    (GMT+08:00) 2018-09-02 15:56:29

    Waziri wa miundo mbinu wa Rwanda Bw. Claver Gatete jana amesema tangu Rwanda na China zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 47 iliyopita, pande hizo mbili zimefanya ushirikiano katika ujenzi wa miundo mbinu, na chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ushirikiano huo umepata maendeleo mapya.

    Bw. Gatete amesema kuwa, China imekuwa mwenzi mkubwa wa kibiashara wa Rwanda, makampuni mengi ya China yameshiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu na utandawazi wa viwanda, kuunga mkono Rwanda kuinua kiwango cha miundo mbinu, kuongeza ajira, kuandaa watu wa kitaaluma, kusukuma mbele utandawazi wa viwanda wa kisasa, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii wa Rwanda.

    "makampuni mengi ya China yamekuja Rwanda hasa katika mawasiliano ya barabara na sekta nyingine za miundo mbinu, wenzi wetu ni pamoja na kampuni ya SINOHYDRO, kampuni ya ujenzi wa uhandisi wa kiraia ya China, kampuni ya barabara na madaraja ya China. Tumefanya mazungumzo na makampuni yenye nia ya kuwekeza katika eneo la viwanda la Rwanda, ambayo yatafanya miradi ya ujenzi katika sekta ya viwanda nyepesi."

    Bw. Gatete amesema nchi za Afrika zikitaka kujiendeleza ni lazima kutatua suala la kurahisisha biashara. Kukamilika kwa Mradi wa reli ya Mombasa na Kigali , hakika kutapunguza gharama ya usafiri, kutainua urahisi wa soko, kutahimiza biashara ya kanda ya Afrika Mashariki, na kutaifanya Rwanda inufaike na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    "hakuna shaka kwamba, tunataka kuunganisha sehemu ya kaskazini ya kanda ya EAC, ili Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC ziunganishwe . Reli ya SGR ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya imekamilika na inafanya kazi . Kwa sasa tumeanza kufanya ujenzi wa reli nyingine, ili tuweze kuwa na mfumo kamili wa reli, na utakaotusaidia kuunganisha njia ya kusafirisha bidhaa za Rwanda, Uganda, Kenya na nchi nyingine kwenda Bandari ya Mombasa, na kupunguza gharama ya usafirishaji wa bidhaa."

    Mwezi Julai mwaka huu, rais Xi Jinping alipofanya ziara nchini Rwanda, China na Rwanda zilisaini mkataba wa safari ya ndege ya abiria. Bw. Gatete amesema hatua hiyo itazisaidia China na Rwanda kushirikiana kujenga mtandao wa safari ya ndege ya kikanda kupata maendeleo mapya.

    "mawasiliano kati ya Rwanda na China ni muhimu sana, tulisaini mkataba wa safari ya ndege ya abiria, kwa hivyo shirika la ndege la Rwanda linaweza kuanzisha safari ya moja kwa moja kwenda China, vilevile, shirika la ndege la China pia linaweza kuanzisha safari ya moja kwa moja kwenda Rwanda. Kwa sasa tunafikiri kuanzisha safari kati ya Kigali na Guangzhou, baadaye tutafikiri safari kati ya Kigali na miji mingine ya China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako