• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa serikali ya Uganda: FOCAC na "Ukanda Mmoja, Njia Moja" vitakuza ushirikiano kati ya nchi yake na China ufikie ngazi mpya

    (GMT+08:00) 2018-09-02 18:21:39

    Naibu msemaji wa serikali ya Uganda Shaban Bantariza amesema urafiki wa jadi kati ya China Uganda ni imara, na anatarajia kuwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" vitahimiza ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana kati ya nchi hizo mbili ufikie kwenye ngazi mpya.

    Alipozungumza na mwandishi wetu wa habari, Bw. Shaban anasema,

    "Urafiki kati ya China na Afrika ni wa siku nyingi, na China ilitoa msaada mwingi kwa nchi za Afrika wakati zikijitafutia uhuru, hivyo pande hizo mbili zimedumisha urafiki mkubwa. Uganda inatarajia kuwa mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika hivi karibuni jijini Beijing utaimarisha ushirikiano kati ya Uganda na China ili kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili."

    Bw. Shaban pia amesifu kazi zinazofanywa na pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika kurahisisha biashara na kuipatia Uganda na nchi nyingine za Afrika fursa za maendeleo, na anatarajia kuwa ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana kati ya nchi hizo mbili utazaa matunda zaidi. Anasema,

    "Baada ya kutolewa kwa pendekezo hilo, mlolongo wa Uganda wa kuagiza bidhaa za China umefupishwa, na ufanisi wa usambazaji wa bidhaa umeongezeka. Kutokana na kufupishwa kwa muda wa usafirishaji bidhaa na kupungua kwa gharama za usafirishaji, bidhaa zilizoagizwa na Uganda kutoka China zimeongezeka na wafanyabiashara wa Uganda wanaojikita katika biashara na China wamepata manufaa halisi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako