• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Afrika Kusini wakutana

    (GMT+08:00) 2018-09-03 07:40:32

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Afrika Kusini rais Cyril Ramaphosa wamefanya mazungumzo kabla ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kukubaliana kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo zao ufikie kwenye ngazi mpya.

    Rais Xi amesema China na Afrika Kusini zinathaminiana, kutendeana kwa urafiki na kuaminiana, na anaamini kuwa ushiriki wa rais Ramaphosa kwenye mkutano huo utaingiza uhai mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na bara la Afrika. Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kufuata malengo yaliyowekwa, kutekeleza kwa juhudi makubaliano muhimu yaliyofikiwa na kutunga mipango ya kimkakati kwa ushirikiano wa pande mbili katika miaka 10 ijayo. Pia amezitaka nchi hizo kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu, kuzidi kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na mawasiliano ndani ya chama na kati ya watu na watu.

    Rais Ramaphosa amesema uhusiano kati ya Afrika Kusini na China umejengwa kwenye msingi wa usawa, kuheshimiana na kunufaishana, ni wa kutegemewa na kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako