• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2018-09-03 09:40:04

    Ofisa mtendaji mkuu wa Idara ya maendeleo ya Rwanda Bw. Emmanuel Hategeka hivi karibuni hapa Beijing amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa Rwanda umeongezeka kwa kasi, na miundo ya uchumi pia imeboreshwa siku hadi siku. Rwanda inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji, na kuwakaribisha wawekezaji wa nje kuwekeza nchini humo. Anasema,

    "Kuwekeza Rwanda kunaweza kufungua soko la Afrika Mashariki, soko la Umoja wa Ulaya na hata soko la Marekani, na wawekezaji wanaweza kunufaika kwenye mchakato wa uwekezaji. Rwanda ina sera nafuu za kuingia sokoni, ikiwemo msamaha wa kodi."

    Alipozungumzia Maonesho ya kimataifa ya Uagizaji bidhaa kutoka nje ya China yatakayofanyika huko Shanghai baadaye mwaka huu, Bw. Hategeka amesema,

    "Tuna matarajio na maonesho hayo, na tunatumai kushirikiana na China kutafuta fursa mpya, na kutangaza bidhaa za nchi yetu, zikiwemo chai, kahawa, madini, na utalii, pia tunawakaribisha marafiki wa China kuwekeza nchini Rwanda. Hii itakuwa ni fursa nzuri ya kuwanufaisha wananchi na kuhimiza maendeleo ya biashara kati ya nchi hizo mbili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako