• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya Afrika Mashariki vyafuatilia mkutano wa kilele wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-09-03 09:43:34

    Vyombo vya habari vya Kenya, Ethiopia, Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki vinaona mkutano wa kilele wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unaoendelea kufanyika hapa Beijing utatoa fursa zisizo na mfano kwa Afrika.

    Gazeti la Daily Nation la Kenya limetoa makala ikisema mbali na miradi mikubwa ya miundombinu ya serikali na bidhaa, China ina mambo mengi mengine ambayo nchi za zinapaswa kujifunza, haswa katika uzalishaji viwandani, kilimo, mipango miji, ulinzi wa mazingira, kuondoa umaskini, uongozi na mfumo wa mawasiliano barabarani.

    Shirika la habari la Ethiopia limesema mkutano wa kilele wa FOCAC unaofanyika Beijing utaimarisha ushirikiano kati ya Ethiopia na China chini ya utaratibu wa Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa Kusini na Kusini, na miradi ya China nchini Ethiopia imeiletea nchi hiyo malaki ya nafasi za ajira, na katika mwaka wa fedha uliopita, China ilitoa msaada wa udhamini wa masomo kwa wanafunzi 2000 wa shahada ya pili na ya tatu wa Ethiopia.

    Gazeti la New Vision la Uganda limesema nchi hiyo itanufaika na mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing ambao unatarajiwa kujadili mchakato wa maendeleo ya kiviwanda barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako