• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa vitendo vinane vya ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 18:08:33

    Baada ya kutoa mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2015, rais Xi Jinping leo amesema, China itashirikiana na nchi za Afrika kuweka mkazo katika kutekeleza vitendo vinane katika miaka mitatu ijayo, kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza maendeleo ya viwanda, kufangamanisha miundombinu, kurahisisha biashara, kujiendeleza bila ya kuchafua mazingira, kujenga uwezo, afya na matibabu, mawasiliano ya utamaduni, na Amani na usalama. Ili kutekeleza vitendo hivyo bila matatizo, China inapenda kutoa dola za kimarekani bilioni 60 kwa Afrika zikiwa ni utoaji wa msaada wa serikali, uwekezaji wa mabenki na makampuni. Pia itasamehe madeni ya mikopo isiyo na riba kati ya serikali na nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, nchi zenye madeni makubwa, nchi zinazoendelea za bara la ndani, nchi zinazoendelea za visiwa vidogo barani Afrika ambayo hayajalipwa mpaka mwishoni mwa mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako