• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yafanya uchaguzi wa wabunge

  (GMT+08:00) 2018-09-03 19:07:13

  Rwanda leo imefanya uchaguzi wa wabunge, ikiwa ni nne kufanyika tangu nchi hiyo ilipofanya uchaguzi wa kwanza baada ya mauaji ya kimbari mwaka 2003.
  Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za huko na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika saa tisa alasiri, na karibu watu milioni 7.1 wanatarajiwa kupiga kura katika vituo zaidi ya elfu 2 nchini humo. Chama tawala nchini Rwanda RPF kilifanya kampeni kwa kutoa ahadi kadhaa ikiwemo kuongeza ajira, mageuzi kwenye kilimo, maendeleo ya sekta binafsi, maendeleo ya miji, na kuimarisha ukuaji wa uchumi.
  Katibu mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Charles Munyaneza amesema, kazi ya kuhesabu kura itaanza mara moja baada ya vituo vya kupigia kura kufunga saa tisa alasiri, na matokeo rasmi yatatangazwa kesho.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako