• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:26:04

    Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa leo hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye mkutano huo. Amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na Afrika kujenga jumuiya yenye mutakabali wa pamoja inayobeba majukumu kwa pamoja, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kusitawisha pamoja tamaduni, kujenga mazingira ya usalama kwa pamoja na kuishi pamoja katika hali ya masikilizano. China itashirikiana na nchi za Afrika kuweka mkazo katika kutekeleza vitendo vinane katika miaka mitatu ijayo, kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza maendeleo ya viwanda, kufangamanisha miundombinu, kurahisisha biashara, kujiendeleza bila ya kuchafua mazingira, kujenga uwezo, afya na matibabu, mawasiliano ya utamaduni, na Amani na usalama.

    Baada ya kujiunga kwa Gambia, Sao Tome na Principe pamoja na Burkina Faso, idadi ya wanachama wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC imefikia 53.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, China siku zote inashikilia kushirikiana na nchi za Afrika kujiendeleza kwa pamoja. Amesema,

    "China na Afrika zimefuata njia yenye umaalumu dhahiri ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, katika ushirikiano kati yake na Afrika, China itashikilia kutoingilia kati utafiti wa nchi za Afrika kuhusu kutafuta njia ya kujiendeleza inayolingana na mazingira yao, kutoingilia mambo ya ndani ya Afrika, kutozilazimisha nchi za Afrika kupokea nia yake yenyewe, kutoweka sharti lolote la kisiasa katika msaada wake kwa Afrika, na kutojitafutia faida binafusi ya kisiasa katika kuwekeza vitega uchumi na kukusanya mitaji kwa ajili ya Afrika."

    Miaka mitatu iliyopita, tangu kufanyika kwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2015, mjini Johannesburg, China imetekeleza kikamilifu mipango kumi ya ushirikiano kati yake na Afrika. Pia imetimiza ahadi yake ya kutoa msaada wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 60 kwa Afrika. Licha ya hayo, baadhi ya ujenzi wa reli, barabara, miundo mbinu na maeneo ya biashara umekamilika na mwingine bado unaendelea. Aidha, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za sayansi, elimu, utamaduni, afya, kuondoa umaskini na kuleta manufaa kwa watu bado unaendelea.

    Baada ya kutoa mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2015, rais Xi Jinping leo amesema, China itashirikiana na nchi za Afrika kuweka mkazo katika kutekeleza vitendo vinane katika miaka mitatu ijayo, kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza maendeleo ya viwanda, kufangamanisha miundombinu, kurahisisha biashara, kujiendeleza bila ya kuchafua mazingira, kujenga uwezo, afya na matibabu, mawasiliano ya utamaduni, na Amani na usalama. Kuhusu kurahisisha biashara, rais Xi amesema,

    "China inaamua kupanua uingizaji wa bidhaa za Afrika haswa bidhaa zisizo za maliasili, kuunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye Maonyesho ya kimataifa ya China kuhusu bidhaa zinazoingizwa kutka nje, kusamehe malipo ya nchi za Afrika zilizoko nyuma zaidi za kimaendeleo kushiriki kwenye maonyesho hayo. Ameongeza kuwa China itaendelea kutekeleza miradi 50 wa biashara huria kwa Afrika, kuunga mkono ujenzi wa maeneo ya biashara huria barani Afrika, kuendelea kufanya mazungumzo na nchi na sehemu za Afrika zenye nia ya kufanya biashara huria, kuhimiza ushirikiano wa biashara ya elektroniki kati ya China na Afrika."

    Ili kutekeleza vitendo hivyo bila matatizo, China inapenda kutoa dola za kimarekani bilioni 60 kwa Afrika zikiwa ni utoaji wa msaada wa serikali, uwekezaji wa mabenki na makampuni. Pia itasamehe madeni ya mikopo isiyo na riba kati ya serikali na nchi zilizoko nyuma kabisa kimaendeleo, nchi zenye madeni makubwa, nchi zinazoendelea za bara la ndani, nchi zinazoendelea za visiwa vidogo barani Afrika ambayo hayajalipwa mpaka mwishoni mwa mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako