• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kudhibiti bei ya Mafuta

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:35:32

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Bw Isack Kamwelwe amesema serikali imejipanga kudhibiti ucheleweshaji wa kupakua shehena ya mafuta bandarini ili kudhibiti kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la ndani.

    Akizungumza mjini Dar es Salaam katika, Kamwele amebaini kuwa wakati wa upakuaji mafuta, kunakuwa na tatizo la ucheleweshaji ambalo mwisho wa siku huchangia kuongezeka bei ya mafuta.

    Amesema wamegundua kuwa uwezo mdogo wa pampu za meli za kupakua mafuta, uhaba wa matangi ya kuhifadhia kwa waagizaji wa bidhaa hiyo pamoja na kuvuja kwa mabomba ya mafuta, ndio chanzo kikubwa cha kupanda bei. Alisema tatizo lingine alilogundua linachangia ucheleweshaji wa kupakua bidhaa hiyo sokoni ni waagizaji wa mafuta, ambao wengi wao huagiza shehena kubwa wakati uwezo wa matangi ya kuhifadhia ni mdogo. Mbaya zaidi, waziri alisema gharama za ucheleweshaji huo hupelekwa kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi. Amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko kufanyia kazi suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako