• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatimaye Nakumatt yaondoka mjini Mombasa

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:35:55

    Kampuni ya maduka ya Nakumatt hatimaye imeondoka katika soko la Mombasa baada ya kufunga tawi lake la mwisho katika eneo la Likoni mjini humo. Kampuni ya Nakumatt ililazimishwa kufunga tawi hilo na Mahakama baada ya kushindwa kumlipa mmiliki wa jengo Kodi. Inadaiwa Nakumatt inadawa kodi ya jumla ya shilingi milioni 107 ambayo imelimbikizika kwa zaidi ya miezi 21. Machi mwaka huu, kampuni hiyo pia ililazimika kufunga tawi lake la Nyali mjini humo baada ya kushindwa kulipa kodi ya shilingi milioni 27.8. Hivi sasa kampuni ya Naivas imechukua nafasi hiyo ya Likoni iliyoachwa na Nakumatt huku kampuni ya Afrika kusini ya Shoprite ikichukua ile ya City Mall mjini Mombasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako