• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta mbalimbali zapongeza hotuba ya rais Xi kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya wakuu wa China na Afrika na wajumbe wa biashara

  (GMT+08:00) 2018-09-04 09:36:11

  Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alitoa hotuba ya "Kuelekea kwa Pamoja Kwenye Ustawi" kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya viongozi wa China na Afrika na wajumbe wa sekta za viwanda na biashara na mkutano wa sita wa wajasiriamali wa China na Afrika uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Beijing wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kusisitiza kuwa China inaziunga mkono nchi za Afrika zishiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, kupenda kufanya kazi na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana, ili kuboresha maisha ya watu. Sekta mbalimbali barani Afrika zimepongeza hotuba hiyo ya rais Xi Jinping, na kuona hotuba hiyo imezielekeza nchi za Afrika kushiriki kwa kina kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kushirikiana na China kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja.

  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya demokrasia na uongozi nchini Kenya Bw. Denis Cody amesema, kuimarisha mawasiliano kunaweza kuzisaidia nchi za Afrika kuondoa umaskini na kutimiza mambo ya kisasa, pia kunaweza kuzihimiza kampuni za China ziende nje ya nchi kufanye biashara. Rais Xi ametaja kujenga njia ya maendeleo yenye kiwango cha juu, hii ni kuisaidia Afrika kupata maendeleo na kutatua suala la kimsingi lililosababisha mgogoro barani humo.

  Mbunge wa Tanzania Dkt. Dalaly Peter Kafumu amesema, China inatoa msaada kwa Afrika na kufanya ushirikiano na Afrika bila masharti ya kisiasa, hili ni jambo kuu kwa Afrika na China kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara bila kusita. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania na China zimepanua ushirikiano kwenye sekta za afya, elimu na uhifadhi wa maji kutokana na ujenzi wa miundo mbinu peke yake. Amesema ana imani kuwa mawasiliano na ushirikiano kati ya Afrika na China unaoimarishwa siku hadi siku hakika utaleta fursa nyingi kwa nchi za Afrika.

  Rais Xi Jinping wa China kwenye hotuba yake amesema, China inawakaribisha wawekezaji wa nchi mbalimbali duniani wakiwemo wawekezaji wa Afrika kuwekeza China, pia inawahimiza wawekezaji wa China kuanza shughuli barani Afrika, na kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja na Njia Moja.

  Mtaalamu wa masuala ya China nchini Nigeria Bw. Charles Onunaiju amesema, anafurahia hotuba ya rais Xi Jinping kuhusu kuzihimiza kampuni za Afrika na China kuwekeza kila upande. Amesema, ongezeko la kampuni za China kuwekeza, kuleta ujuzi na uzoefu wa usimamizi barani Afrika, kampuni za Afrika zitanufaika na kupata maendeleo ya kasi, hivyo bidhaa nyingi zaidi zilizotengenezwa na nchi za Afrika zitaingia kwenye soko la kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako