• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya rais Xi Jinping yathibitisha ushirikiano wa kirafiki na kindugu kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-04 10:22:14

    Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika . Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Somalia Bw. Ahmed Isse Awad amesema hotuba ya rais Xi imethibitisha ushirikiano wa kirafiki na kindugu kati ya China na Afrika.

    Waziri Awad amesema, kwenye ufunguzi wa mkutano huo rais Xi ametangaza mpango wa miaka mitatu ijayo wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na kwamba Somalia inaikaribisha China kushiriki kwenye ukarabati wa Somalia baada ya vita, na kutarajia kuimarisha ushirikiano na China kupitia baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, Akisema,

    "Hotuba ya rais Xi Jinping ina maana ya kihistoria, inawatia watu moyo, inawathibitishia viongozi wa nchi za Afrika na watu wake kwamba ushirikiano kati ya China na Afrika ni wa kindugu, ni uhusiano wa kudumu wa kuzinufaisha pande zote. Kama rais Xi alivyosema katika hotuba yake, tunajenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja yenye nguvu na uhusiano wa karibu. Hii ni hotuba ya kufurahisha, kutia moyo, na inayotupia macho siku za mbele. Mimi na mawaziri wenzangu wa mambo ya nje wa nchi za Afrika tunakubali kuwa hotuba ya rais Xi Jinping imethibitisha uhusiano mkubwa na ushirikiano wa kunufaisha pande zote za China na Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako