• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mke wa rais wa China ahudhuria mkutano wa China na Afrika wa kukinga na kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI

    (GMT+08:00) 2018-09-04 16:48:40

    Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan leo amehudhuria mkutano wa China na Afrika wenye mada ya kushirikiana kukinga ugonjwa wa UKIMWI uliofanyika hapa Beijing.

    Akihutubia mkutano huo, Bibi Peng amepongeza nchi za Afrika kwa kupata mafanikio katika kukinga na kudhibiti maambukizi ya UKIMWI, na kueleza mafanikio na uzoefu mzuri wa China katika kukabiliana na ugonjwa huo. Bibi Peng amesema, kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI ni lengo la pamoja la jamii ya kimataifa, na China na Afrika zimepata mafanikio katika ushirikiano wa kudhibiti ugonjwa huo.

    Amesema kuanzia mwaka ujao, China itashirikiana na nchi za Afrika na mashirika husika ya kimataifa kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa kukinga ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana wa pande hizo mbili na kuhimiza afya ya mitaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako