• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika akana msukosuko wa madeni barani humo

    (GMT+08:00) 2018-09-04 18:30:16

    Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Akinwumi Adesina amesema, Afrika haina msukosuko wa madeni.

    Bw. Adesina amesema hayo baada ya kushiriki kwenye mkutano wa sita wa wafanyabiashara wa China na Afrika. Amesema, katika siku za karibuni, uwiano wa madeni na pato la taifa la nchi za Afrika umeoongezeka kwa kiasi kidogo. Mwaka 2017, idadi hiyo ilifikia asilimia 37 kutoka asilimia 22 ya mwaka 2010, lakini bado iko chini ikilinganishwa na idadi ya juu ya asilimia 100 hadi 150 ya baadhi ya nchi zilizoendelea.

    Bw. Adesina amesisitiza kuwa, ujenzi wa miundombinu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi za Afrika, lakini nchi hizo bado ziko nyuma katika sekta hiyo ambayo itachangiwa kutokana na mradi wa ujenzi wa miundo mbinu chini ya pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako