• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Mambo manane" yafuatiliwa zaidi kwenye ushirikiano wa mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:27:14

    Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Xu Jinghu leo amesema, mambo manane yaliyotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing yameeleza njia halisi ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika, na yanafuatiliwa zaidi kwenye ushirikiano wa mkutano huo.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Xu amesema mambo hayo manane yaliyotolewa kwenye mkutano huo na mipango 10 ya ushirikiano iliyotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg yana uhusiano wa karibu na wa mfululizo, pia yataleta manufaa zaidi kwa watu wa pande mbili za China na Afrika.

    Bw. Xu amesema, mambo hayo yanaendana na ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na mkakati wa jumla wa maendeleo ya Afrika, na yataharakisha ustawi wa uchumi wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako