• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Kampuni 8 zawasilisha maombi ya kujenga barabara ya Kampala-Jinja

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:35:56

    Mamlaka ya barabara ya kitaifa ya Uganda (Unra) imechapisha majina ya kampuni 8 ambazo zimewasilisha maombi ya kupewa kandarasi ya kujenga barabara kuu kati ya mji mkuu Kampala na Jinja.

    Mamlaka hiyo imesema itachunguza maombi hayo ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.

    Mkurungezi wa Unra Allen Kagina amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi ili kuongeza njia za ufadhili.

    Baadhi ya kampuni ambazo zimewasilisha maombi ni pamoja na China Communications /China First Highway Engineering na Vinci Concessions.

    Maafisa wa Unra wamesema gharama ya mradi huo inatarajiwa kuwa dola bilioni 1 na serikali tayari imetoa dola milioni 400 kwa ujenzi wa barabara hiyo ya urefu wa kilomita 95.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako