• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu za Afrika Mashariki zaimarisha maandalizi

  (GMT+08:00) 2018-09-05 09:58:26

  Kuelekea michezo yake ya kufuzu mashindano ya AFCON ya mwaka 2019 itakayofanyika mwishoni mwa juma hili, timu za Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi zimeendelea na maandalizi kwa nyakati tofauti ili kukabiliana na upinzani.

  Burundi maarufu kama Intamba mu Rugamba ambao wanajiandaa na mechi dhidi ya Gabon wameendelea na mazoezi chini ya kocha mkuu Olivier Niyungeko, ambaye hivi karibuni aliwaita kikosini wachezaji wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi, akiwemo Christopher Nduwarugira anyecheza katika klabu ya Uniao de Madeira ya Ureno.

  Harambee Stars, timu ya taifa ya Kenya wao wameenda mbali zaidi kuita nyota wote wanaocheza ligi za kulipwa barani ulaya, kwa kusudi moja tu, ambalo ni kutokana ugumu wa mechi inayowakabili dhidi ya Ghana ambayo licha ya kuwa miongoni mwa timu bora Afrika, nayo pia imejipanga na iko kambini nchini Ethiopia ili kuzoea mazingira ya mashariki.

  Kwa upande wake kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, Vincent Mushami amesema licha ya kumkosa mshambuliaji wake namba moja Jacques Tuyisenge ambaye ni majeruhi, ana imani na wachezaji wengine kuziba pengo lake akiwemo Meddie Kagere, na amewataka mashabiki wa timu hiyo kuunga mkono na kuendelea kuamini wachezaji wa timu hiyo kwa sasa kwani kiwango chao ni tofauti na miaka iliyopita.

  Nchini Tanzania, tayari mchezaji na nahodha wa timu Mbwana Samata amewasili ili kukiongeza nguvu kikosi cha kocha Emanuel Amunike kinachotarajiwa kuumana na timu ya taifa ya Uganda ambao ndiyo tishio kubwa kwa nchi za Afrika Mashariki, nayo pia iko kambini chini ya kocha mkuu wake Sebastien Desabre ambaye anakabiliwa na shinikizo la kuipatia mafanikio timu hiyo.

  Mechi za kufuzu Afcon zinafanyika Septemba 8 na septemba 9 na mashindano ya Afcon yanatarajiwa kufanyika mwezi januari mwaka 2019 nchini Cameroun.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako