• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Ufaransa ajitahidi kuondoa hali ngumu ya Umoja wa Ulaya

  (GMT+08:00) 2018-09-05 17:46:20

  Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ambaye ni mmoja wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, mwishoni mwa mwezi Agosti, alihutubia mkutano wa mabalozi wa Ufaransa katika nchi za nje, akitetea msimamo wa pande nyingi, na kuonyesha kuwa Ufaransa inajitahidi kuongoza Umoja wa Ulaya kujiondoa kwenye hali ngumu.

  Rais Macron amesema msimamo wa kimataifa wa pande nyingi na maendeleo ya Umoja wa Ulaya vinakabiliwa na hali ngumu ambayo haikuwepo zamani. Amesema pamoja na viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya kufanya mawasiliano na Marekani, lakini msimamo wa upande mmoja wa serikali ya Marekani haujabadilika. Rais Donald Trump wa Marekani hawezi kuvumilia Ulaya kuchukua maslahi ya Marekani katika mawasiliano kati yake na Marekani. Vita ya kibiashara inaendelea dhidi ya Umoja wa Ulaya, pia inatoa shinikizo kwa malipo ya ada kwa nchi za Ulaya ambazo ni wanachama wa NATO, na kuitaka Ulaya kurudisha maslahi yake ya kiuchumi.

  Kwenye mkutano na mabalozi wa Ufaransa katika nchi za nje, rais Macron amefafanua njia zitakazotumiwa na Ufaransa katika kukabiliana na hali ya kimataifa na masuala mengine nyeti. Amelaani kitendo cha upande mmoja cha Marekani, pia ameeleza ulazima wa kufanya mazungumzo na Marekani, na kukubali ushiriki wa China katika uhusiano wa pande nyingi.

  Kuhusu utawala wa dunia, rais Macron anaona kuwa, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lina umuhimu wa kutuliza baadhi ya sehemu na dunia, na Ufaransa inashikilia kanuni ya kujipatia uwiano na kulinda maslahi yenyewe, pamoja na kufanya mazungumzo ya kiujenzi na China.

  Anashikilia lengo la maendeleo yenye kigezo cha juu la utandawazi wa Umoja wa Ulaya, kupinga mwelekeo wa ufarakanishaji ndani ya Umoja huo na kuhimiza mageuzi na kusaidiana katika Umoja huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako