• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Kusini yasema mazungumzo ya amani yanakaribia kumalizika

  (GMT+08:00) 2018-09-05 20:04:51

  Pande zinazopingana nchini Sudan Kusini zimeafikiana kuhusu chanzo cha kutekeleza makubaliano ya amani, hivyo kutoa njia kwa kusainiwa kwa makubaliano ya mwisho katika siku za karibuni.

  Msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Michael Makuei amesema, mazungumzo yanayoendelea nchini Sudan yatahitimishwa baada ya pande zinazopingana kufikia makubaliano juu ya masuala muhimu katika pendekezo la mwanzo la amani. Amesema wasimamizi kutoka shirika la kikanda la IGAD wameandaa semina elekezi ya siku tatu kwa pande hizo ili kuelewa vizuri makubaliano hayo, na hatua hiyo itaashiria kumalizika kwa majadiliano kuhusu makubaliano ya amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako