• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya biashara ya huduma Kati ya China na nchi za nje katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu yafikia yuan trilioni 2.9

    (GMT+08:00) 2018-09-05 20:10:05

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zimeonyesha kuwa, katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara ya huduma ya China kwa nchi za nje imeongezeka kwa asilimia 9.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo na kufikia yuan trilioni 2.9, sawa na dola bilioni 424.6 za kimarekani..

    Naibu mkurugenzi wa idara ya biashara ya huduma ya wizara hiyo Bw. Li Yuan amesema kuwa, baada ya China kuanza kutumia chapa ya kitaifa ya "huduma ya China", uuzaji wa huduma umeendelea kudumisha ongezeko la kasi. Ongezeko hilo la mwezi Julai limezidi asilimia 20, na uuzaji wa huduma katika mawasiliano ya habari, kampyuta na habari umeongezeka kwa kasi zaidi na kufikia asilimia 50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako