• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Uganda wakutana

    (GMT+08:00) 2018-09-06 17:16:42

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na rais Yoweri Museveni wa Uganda.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi amesisitiza kuwa rais Museveni ni mhimizaji na mshiriki wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na alitoa mchango muhimu kwa ujenzi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema China siku zote inaona Uganda ni rafiki muhimu katika kufanya ushirikiano barani Afrika, na inapenda kushirikiana na nchi hiyo kwenye msingi wa kutekeleza pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na mafanikio ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC. Pia kuimarisha usimamizi na utawala wa nchi, hasa kubadilishana uzoefu wa mbinu za kupunguza umaskini, kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu, kuisaidia Uganda kuharakisha mchakato wa viwanda, na kuimarisha ushirikiano wa huduma za jamii.

    Rais Museveni ameshukuru juhudi za Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China kwa kuzisaidia nchi za Afrika kuendeleza uchumi wao. Amesema Uganda inataka kushirikiana na China katika sekta ya mawasiliano na usafirishaji, maeneo ya viwanda, nishati na kuimarisha mawasiliano kati ya pande hizo mbili katika mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako