• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Uhaba wa mafuta waendelea kushuhudiwa siku ya pili .

    (GMT+08:00) 2018-09-06 19:30:45

    Uhaba wa mafuta katika vituo vya uuzaji wa mafuta jijini Nairobi, umeendelea kushuhudiwa kwa siku ya pili hii leo ,baada ya muungano wa wafanyibiashara wa mafuta nchini kugoma kufikisha mafuta hayo vituoni.

    Licha ya juhudi za wizara ya kawi nchini Kenya kutaka biashara hiyo iendelee kama kawaida,wadau hao wamesisitiza kuendelea na mgomo huo hadi pale serikali itakapoondoa ushuru ,wa asilimia 16 kwa bidhaa za petroli.

    Washikadau hao wamedai kwamba ushuru huo umeathiri biashara zao na kuwalazimu kusaka fedha zaidi za mtaji wa kuagiza mafuta.

    Kodi hiyo ya asilimia 16 ilitangazwa na wizara ya fedha, licha ya mswada uliopitishwa na bunge ambao ulitupilia mbali kodi hiyo kwa miaka miwili.

    Mililongo mirefu ya watumiaji wa magari binafsi imeonekena katika vituo vya kuuza mafuta jijini, jambo lililopelekea kwa uuzaji wa mafuta kwa viwango finyu.

    Wakenya wengi wamekuwa wakielezea hasira zao kutokana na hali inayojiri huku wengine wakilazimika kufunga foleni ndefu katika vituo vya mafuta .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako