• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia:Ethiopia kuboresha mtaji wa binadamu

    (GMT+08:00) 2018-09-06 19:32:15

    Serikali ya Ethiopia imetangaza kushirikiana na sekta binafsi pamoja mashirika ya kimataifa kuimarisha maendeleo ya jamii na kupunguza umaskini.

    Kupitia kwa vyombo vya habari ,waziri mkuu Abiy Ahmed amejitolea kuhakikisha kwamba fedha walizopata kutoka kwa benki ya dunia zitatumika ipasavyo kufufua miradi muhimu ya kumaliza umaskini.

    Ethiopia imepewa dola bilioni moja na benki kuu ya dunia zisaidie kwenye bajeti yake .

    Msaada huu ulijiri kufuatia kikao cha Abiy na Jim Young Kim ,rais wa benki ya dunia.

    Bw Jim aliahidi kuisaidia zaidi Ethiopia baada ya kuitelekeza kwa mda mrefu .

    Ethiopia ina bajeti ya dola bilioni 1.89 zilizotoka kwenye misaada na mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako