• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kampuni za bima kubuni mbinu za kuvutia wateja

    (GMT+08:00) 2018-09-06 19:33:58

    Mpango wa hazina ya kitaifa ya bima ya huduma za matibabu (NHIF), umechukua sehemu kubwa ya biashara ya bima za watu binafsi.

    Hayo ni kulingana na mukurugenzi mkuu wa muungano wa wamiliki wa kampuni za bima nchini- (A.S.K), Tom Gichuhi, ambaye alisema wamiliki hao wa kampuni za bima, sasa wanatafuta njia mpya za kuvutia na kudumisha wateja.

    Ripoti ya mwaka 2017 kuhusu biashara ya bima, inaonyesha kwamba biashara hiyo kwa ujumla haijapenya humu nchini, ambapo ilididimia kwa kiwango fulani hadi asilimia 2.71.

    Kwa upande mwingine, mtaji wa sekta hiyo uliandikisha ukuaji wa asilimia 6.45 hadi shilingi bilioni-209.70 mwaka 2017 kwa kulinganisha na bilioni 197 mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako