• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tanzania yafuzu bila jasho fainali za soka ufukweni.

    (GMT+08:00) 2018-09-07 09:22:07

    Timu ya taifa ya soka la ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Misri, kufuatia waliokuwa wapinzani wao kwenye mechi ya mchujo, Afrika Kusini kujitoa.

    Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limewajulisha TFF juu ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi nane.

    Mchezo mwingine utakuwa kati ya timu ya taifa ya soka ya ufukweni ya Uganda (Sand Cranes) imeanza maandalizi ya kumenyana na Cote d'Ivoire kutafuta nafasi ya kufuzu fainali ya Afrika, itakayofanyika nchini Misri mwezi Desemba.

    Mataifa nane, yatashiriki katika fainali hizo za bara Afrika na hadi sasa, wenyeji Misri, Libya, Morocco, Nigeria na Senegal tayari yameshafuzu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako