• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Acacia kuwajengea uwezo wataalamu wa madini

    (GMT+08:00) 2018-09-07 18:42:26

    Kampuni ya Acacia imeingia makubaliano ya kuwajengea uwezo watalaamu wa madini nchini baada ya kusaini makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

    Katika utekelezaji wa makubaliano hayo, kampuni hiyo inayoongoza kwa uchimbaji wa dhahabu itakuwa inawafadhili wanafunzi na walimu wa chuo kikuu hicho kuhakikisha wanapewa maarifa yanayohitajika.

    Kwenye utiaji saini wa makubaliano hayo, Acacia imetoa ufadhili wa masomo kwa baadhi ya wataalamu nchini Canada katika Chuo Kikuu cha Alberta.

    Akizungumza katika mkutano wa kusaini mkataba huo, mkurugenzi mtendaji wa Acacia, Asa Mwaipopo amesema mbali na ufadhili huwa wanatoa nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa uhandisi wa madini katika migodi yao ili kuwaongezea ujuzi.

    Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Acacia kutoa ufadhili wa aina hiyo. Mwaipopo anasema hatua waliochukua itafungua milango kwa watu wengine kusaidia kujenga jukwaa la maendeleo. Ufadhili uliotolewa ni wa jumla ya Dola 60,000 za Marekani (sawa na Sh137 milioni)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako