• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wa kahawa Uganda walalamikia kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo

    (GMT+08:00) 2018-09-07 18:43:36

    Wawekezaji wa kahawa nchini Uganda wanaendelea kulalamikia kushuka kwa mapato ya zao hilo kufuatia kushuka kwa bei ya zao hilo kwenye soko la kimataifa. Akizungumza na radio China kimataifa, mkuu wa maendeleo endelevu katika Umoja wa Ulaya Bw Aloys Lorkeers amesema bei ya zao hilo imekuwa ikiteremka kwa muda wa wiki tatu sasa.

    Kwenye mnada wa kahawa, kilo moja ya bidhaa hiyo imeshuka kutoka shilingi 2,300 hadi 1,500.

    Hivi sasa mamlaka husika nchini Uganda imeahidi kufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa nchi hiyo inazalisha magunia milioni 20 kutoka milioni 3 ya hivi sasa. Uganda imesema hivi sasa inalenga kuhakikisha kuwa bei ya bidhaa hiyo inadhibitiwa ili kuwasaidia wawekezaji wa zao hilo. Sekta ya binafsi tayari imeonesha nia ya kuingia kwenye kilimo cha zao hilo ili kupiga jeki sekta hiyo nchini Uganda. Uganda huuza kahawa yake barani Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako