• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: Manangoi na Chepkoech kutoka Kenya waibeba Afrika mashindano ya mabara

    (GMT+08:00) 2018-09-10 10:14:09

    Bingwa wa michezo ya jumuiya ya madola ambaye pia ni bingwa wa dunia wa mbio za mita 1500 Elijah Manangoi wa Kenya, jana ameshinda nafasi ya kwanza akiliwakilisha bara la Afrika kwenye mashindano ya mabara duniani yaliyoandaliwa na IAAF nchini Jamhuri ya Czech.

    Manangoi ambaye pia ni bingwa wa Afrika, alishinda mbio hizo baada ya kutumia dakika 3 na sekunde 40.

    Beatrice Kepkoech kutoka ambaye ni bingwa anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za wanawake za mita 3000 za kuruka vihunzi, jana pia aliibeba 'Team Africa' kwa kushinda nafasi ya kwanza ya kipengele hicho, ambapo pia aliweka rekodi mpya tena kwa kutumia dakika 9, sekunde 7 na nukta 92.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako