• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi ya mataifa ya Ulaya: Mbappe azidi kung'ara na Ufaransa yake

    (GMT+08:00) 2018-09-10 10:15:02

    Katika kuendelea kuonyesha makali yake, Kylian Mbappe amefunga goli la kwanza la ushindi wa magoli 2-1 iliyopata timu ya taifa ya Ufaransa ilipocheza dhidi ya Uholanzi kwenye mechi yake ya ligi ya soka kwa mataifa ya Ulaya.

    Mbappe alifunga goli hilo katika dakika ya 14, lakini Uholanzi wakasawazisha kupitia Ryan Babel kunako dakika ya 67 kabla ya Olivier Giroud kufunga goli la pili la Ufaransa katika dakika ya 80.

    Katika mechi zingine zilizopigwa jana, Denmark ilipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wales, Ukraine ikashinda 1-0 dhidi ya Slovakia, Norway ikifungwa 1-0 na Bulgaria, na Cyprus ikapata ushindi mnono dhidi ya Slovenia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako