• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, kufuzu Afcon 2019: Matokeo ya timu za Afrika Mashariki

  (GMT+08:00) 2018-09-10 10:17:15

  Mwishoni mwa juma lililopita, timu za soka za mataifa ya Rwanda, Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda zilicheza michezo ya raundi ya pili ya mechi za hatua ya makundi ya kufuzu mashindano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019.

  Rwanda ambayo iko kundi H, ikiwa nyumbani jana, ilipoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Ivory Coast ambapo sasa inabaki bila ya pointi hata moja kwa kuwa hata katika mechi ya kwanza ilifungwa na timu ya Jamhuri ya Afrika ya kati, na katika mechi ijayo itacheza dhidi ya Guinea.

  Katika mechi zilizopigwa juzi, Burundi ambayo iko kundi C, ilipata sare muhimu ya magoli 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Gabon. Timu hiyo sasa inafikisha alama 4 kwani kwenye mechi ya kwanza ilishinda dhidi ya Sudan Kusini, na katika mechi ya tatu itakuwa ugenini kucheza na Mali.

  Furaha kubwa zaidi ilikuwa kwenye mechi ya kundi C mjini Nairobi, ambapo Kenya walipata ushindi wa kurejesha matumaini wa goli 1-0 dhidi ya Ghana, na timu hiyo sasa inakuwa na alama 3 sawa na timu nyingine tatu katika kundi hilo kwani kila moja imeshinda mechi moja na kufungwa moja. Katika mechi iliyopita Kenya ilifungwa na Sierra Leone, aidha timu hiyo sasa itakutana na Ethiopia katika mechi inayofuata.

  Katika kundi L timu mbili za Afrika Mashariki, Uganda iliyokuwa nyumbani ililazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania, sare ambayo inaifanya Uganda ifikishe alama 4 kwenye msimamo kwa kuwa ilishinda mechi ya kwanza dhidi ya Cape Verde, lakini Tanzania inakuwa pointi 2 kutokana na sare nyingine kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Lesotho. Uganda sasa inatarajiwa kukutana na Lesotho katika mechi ijayo na Tanzania ikicheza dhidi ya Cape Verde.

  Mechi za raundi ya tatu za michuano hiyo zinatarajiwa kupigwa kati ya Oktoba 10 hadi Oktoba 13.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako