• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ongezeko la thamani ya biashara ya utoaji wa huduma nchini China laleta manufaa makubwa

  (GMT+08:00) 2018-09-10 18:40:52

  Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa biashara ya utoaji wa huduma imefikia dola za kimarekani bilioni 437.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Wakati biashara ya dunia ikikabiliwa na vitendo vya kujilinda kibiashara, thamani ya biashara ya utoaji wa huduma ya China inadumisha ongezeko la asilimia 10, na kuonesha kuwa mwelekeo wa kupata ukuaji wa uchumi kwa hatua madhubuti umeimarika nchini China.

  Biashara ya utoaji wa huduma, ikiwa ni msukumo mpya wa biashara ya nje na ukuaji wa uchumi wa China, maendeleo yake ya kasi yana umuhimu mkubwa kwa China na dunia nzima. Hii imeonesha kuwa mwelekeo wa maendeleo yasiyo na uwiano katika uagizaji na uuzaji wa biashara hiyo yaliyodumishwa kwa muda mrefu yanatarajiwa kuboreshwa, hali ambayo itasaidia China katika kuongeza uwezo wake katika kukabiliana na changamoto mbalimbali, na kuinua kiwango cha sekta hiyo kifikie kile cha kimataifa. Aidha China imekuwa mfano mzuri katika ujenzi wa mfumo wa kurahisisha njia za kufanya biashara ya utoaji wa huduma, ambao utaweza kueneza kote nchini, na kuhimiza biashara ya sekta hiyo ianzishwe nje ya China.

  Mbali na hayo kuboreshwa kwa biashara ya utoaji wa huduma pia kumetoa msukumo mpya kwa kuboresha muundo wa uchumi na kutimiza maendeleo yenye ubora wa juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako