• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chuo kilichojengwa kwa msaada wa China chasaidia kuboresha mafunzo ya kiufundi Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-09-11 09:39:34

  Chuo cha mafunzo ya kiufundi cha IPRC Musanze,nchini Rwanda,kilichojengwa kwa msaada kutoka serikali ya China chasaidia kuwapa vijana wengi taaluma na mafunzo mbalimbali ya kiufundi,na hatimaye kuziba pengo la mahitaji ya soko.

  Chuo hiki kimejengwa na kampuni ya China-Geo Engineering Corporation kwa kutumia U$12m zilizotolewa na serikali ya China.

  Aidha serikali ya China imetoa U$16M zaidi kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho cha IPRC Musanze.

  IPRC Musanze ndio chuo kikubwa zaidi cha kiufundi katika mkoa wa kaskazini mwa Rwanda.Chuo hiki kilianzishwa rasmi mwaka 2015,na kufikia sasa kina wanafunzi 1,200 wanaofanya mafunzo ya kiufundi kama vile Kilimo na usindikaji wa Chakula,umwagiliaji mashamba,uhandisi,ujenzi na utalii.

   

  Mwalimu Mkuu wa Chuo cha IPRC Musanze,Emile Abayisenga,ambaye alisomea nchini China anasema kuwa kupitia ushirikiano wa China na Rwanda,chuo cha IPRC Musanze kimesaidia kuinua maisha ya wakazi wa kijiji cha Barizo eneo la Musanze,na pia kusaidia katika kuongeza idadi ya watu wanaopta mafunzo ya kiufundi nchini Rwanda.

  "Rwanda ina mpango kuwa wanafunzi asilimia 60 wawe wanafanya mafunzo ya kiufundi na asilimia 40 wafanye kozi nyenginezo,lakini bado ni vigumu kufikisha asilimia 60 kwa sababu vifaa na masomo yenyewe ya TVET bado ni machache lakini msaada huu unakuja sasa kusaidia serikali ya Rwanda kupata asilimia 60 kufanya masomo ya kiufundi kwa sababu ndio njia pekee ya kupata ajira na kutengeza ajira"

  Aidha alisema chuo cha IPRC Musanze kina ushirikiano na Chuo cha kiufundi cha Jinhua Polytechnic cha China.

  "Tuna ushirikiano wa mitindo miwili.ushirikiano wa kwanza ni wa serikali ya China yenyewe.Hata hivi tuna mpango wa kupanua chuo chetu.Tulijenga chuo hiki kwa msaada wa China wa U$12M .Serikali ya China imetuongeza $16m za upanuzi.Tuna ushirikiano na Chuo cha Kiufundi cha Jinhua cha China.Wanatusaidia kuongeza uwezo kwa walimu wetu na wanafunzi.Mwezi wa 10 walimu wetu watatu wataenda China katika chuo cha Jinhua kwa mafunzo zaidi"

   

  Eric Shimimana ni mwanafunzi anayejifunza uhandisi wa ujenzi katika chuo cha IPRC Musanze.Anasema msaada wa China wa ujenzi wa chuo hiki hauwanufaishi tu wanafunzi,bali chuo hiki kimekuwa neema kwa watu wengi wa Rwanda,na hasa wakazi wa kijiji cha Barizo.

  "Inaleta manufaa mengi kwa sababu watu wengi wanaoishi karibu na chuo wanapata kazi na misaada mbalimbali"

  Ndekezi Annick ni mwalimu anayefunza upishi na uandaaji wa chakula.Nimempata akiwa jikoni akiwaelekeza wanafunzi wake kuhusu upishi wa mikate.

  Anasema mafunzo wanayowapatia wanafunzi katika chuo hiki yanawaandaa kwa mahitaji ya soko na uanzishaji biashara.

  Mkuu wa Idara ya kilimo katika Chuo cha IPRC Musanze,Sekarigenge Francois anasema ana imani kwamba China itaisaidia Rwanda na Afrika kwa ujumla kuweza kujitosheleza kwa Chakula kwa kutoa mafunzo na vifaa vya kisasa vya kilimo.

  "Kwa sasa Afrika hatujakumbatia teknolojia mpya za kilimo labda kutokana na ukosefu wa pembejeo.Tunafurahia sana mchango wa Rais wa China katika kuendeleza kilimo Afrika,haswa Rwanda.Na tuna imani kuwa tutajifunza kutoka kwao na kuimarisha sekta ya kilimo,na hatimaye kujitosheleza kwa chakula"

  Chuo cha IPRC Musanze ni mojawapo ya misaada mingi inayotolewa na China kwa nchi za Afrika.

  Katika mkutano mkuu wa FOCAC wa mwaka 2015 miongoni mwa mambo mengine,Rais wa China Xi Jin Ping aliahidi kuboresha Viwanda,kilimo cha kisasa,huduma za fedha,maendeleo ya nishati ya kijani,uwezeshaji,biashara na uwekezaji,afya ya umma,na amani na usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako