• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo Kikuu cha Redio na Televisheni cha China chapata maendeleo ya muunganiko wenye uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2018-09-11 09:41:38

    Kituo Kikuu cha Redio na Televisheni cha China kinachoundwa na Televisheni ya Taifa ya China CCTV, Radio ya Taifa ya China CNR na Radio China Kimataifa CRI kimepata maendeleo ya muunganiko wenye uvumbuzi, ambapo nguvu zake za uenezi, ushawishi na uaminifu zimeongezeka kwa kasi, maendeleo ya muunganiko wa vyombo vya habari ni makubwa na kiwango cha utazamaji na nguvu za uenezi za mtandao wa internet zinaongezeka.

    Baada ya kuzinduliwa kwa Kituo Kikuu cha Redio na Televisheni cha China Aprili, 19, watangazaji wa vituo vitatu walitangaza moja kwa moja kwa ushirikiano katika mikutano ya mwaka huu ya Baraza la Bo'ao la Asia. Kampuni iliyo chini ya Kituo Kikuu hicho ilisaini mikataba na kampuni ya teknolojia ya Alibaba na kampuni ya mawasiliano ya simu ya China Mobile kwa malengo ya kusambaza vipindi vyake katika mitandao na sekta nyingine za teknolojia ya hali ya juu.

    Mbali na muunganiko wa habari na vipindi, Kituo Kikuu hicho kimeunganisha nguvu za uenezi za ustawi wa jamii na kutenga Yuan zaidi ya bilioni 1 kutoka kwenye faida za matangazo kusaidia sehemu nyingine zaidi kuondokana na umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako