• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Jinja yapandishwa hadhi kuwa jiji

  (GMT+08:00) 2018-09-11 18:54:26

  Baraza la wilaya ya Jinja nchini Uganda limeidhinisha kupandishwa hadhi ya mji wa Jinja kuwa jiji.

  Mswada wa kupandisha hadhi hiyo ulikuwa umependekezwa na kiongozi wa shughuli za serikali wilayani Jinja bibi Florence Asio na kuungwa mkono na madiwani wote.

  Jiji hilo sasa litajumuisha manisapaa za Kagoma, Butembe na Jinja.

  Meya wa manispaa ya Jinja Majid Batambuze amesema ueneaji wa miji ni njia moja ya kusaidia Uganda kufikia hadhi ya uchumi wa wastani.

  Baadhi ya matakwa iliotakiwa kutimiza Jinja kabla ya kuwa jiji ni pamoja na uwezo wa kutoa huduma, maji ya kutosha na kuwa na idadi ya wakaazi zaidi ya 500,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako