• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zimbabwe: Waziri mpya wa fedha Zimbabwe aahidi kufufua uchumi

  (GMT+08:00) 2018-09-11 18:55:33

  Waziri mpya wa fedha wa Zimbabwe Mthuli Ncube, amesema anapanga kurejesha sarafu ya dola ya Zimbabwe na kuharakisha mipango ya kulipa madeni ya nchi katika juhudi za kufufua uchumi wan chi hiyo.

  Zimbabwe iliacha kutumia fedha zake kati ya mwaka wa 2008 na 2009 baada ya kukumbwa na mfumko mkubwa wa bei wakati wa utawala wa rais Robert Mugabe.

  Waziri Ncube, mwenye umri wa miaka 55, amesomea chuo kikuu cha Oxford na kuhudumu kama makamu wa rais wa benki ya maendeleo ya Afrika.

  Rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa, ameapa kurejesha uchumi wan chi hiyo ambayo wakati mmoja ilikuwa ndio yenye kuzalisha chakula kingi barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako