• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Uganda: Ukaguzi wa viwanja kwa ajili ya msimu mpya wa ligi waanza

    (GMT+08:00) 2018-09-12 11:18:33

    Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda FUFA jana limeanza kufanya ukaguzi wa viwanja vitakavyotumika kwenye msimu wa 2018/2019 ligi kuu na ligi daraja la pili.

    Ukaguzi huo ni wa siku tatu na umeanza jana kwa viwanja 19 kukaguliwa, leo utaendelea kwa viwanja 12, na utahitimishwa kesho.

    Mambo muhimu yanayozingatiwa ni pamoja na ubora wa eneo la kuchezea, uwepo wa eneo kukaa mashibiki, usalama, usafi wa mazingira, umiliki wa uwanja na mikataba ya matumizi, na uwepo wa mawasiliano ya simu na mtandao wa internet.

    Miongoni mwa timu na viwanja ni timu mbili pekee, Vipers na Onduparaka ndiyo zinamiliki viwanja vyake zenyewe lakini zingine hutumia viwanja kwa mkataba wa kukodisha.

    Ligi kuu nchini Uganda ya msimu wa 2018/2019 inatarajiwa kuanza wiki ijayo Septemba 18, na tarehe rasmi ya ligi daraja la pili itatangazwa hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako