• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Ligi ya mataifa ya Ulaya: Hispania yashinda kwa magoli 6-0 dhidi ya Croatia

  (GMT+08:00) 2018-09-12 11:19:32

  Timu ya taifa ya Hispania imeendeleza makali yake kwenye michuano ya ligi ya mataifa ya Ulaya kwa kupata ushindi mnono wa magoli 6-0 ikiwa nyumani jana usiku dhidi ya Croatia kwenye mjini Elche.

  Magoli ya Hispania yalifungwa na Samuel Niguez, Marco Asensio, Rodrigo, Sergio Ramos, Isco na jingine moja likiwa ni la kujifunga wenyewe Croatia kupitia Lovre Kalinic.

  Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Hispania, kwani katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi walishinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Uingereza.

  Katika mechi zingine zilizopigwa jana, Ubeligiji ilishinda kwa magoli 3-0 ilipocheza dhidi ya Iceland, ikifunga kupitia Romelo Lukaku aliyefunga mawili na Eden Hazard aliyefunga moja kwa njia ya Penati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako