• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa biashara na uwekezaji kati ya China na nchi za ASEAN wafunguliwa mjini Nanning

    (GMT+08:00) 2018-09-12 16:22:42

    Mkutano wa kilele wa 15 wa uwekezaji na Biashara kati ya China na Jumuiya ya uchumi ya nchi za Asia Kusini mashariki ASEAN umefunguliwa leo asubuhi mjini Nanning mkoani Guangxi. Kwenye hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, naibu waziri mkuu wa China Bw Han Zheng amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili ili kujenga jumuiya yenye mustakbali wa pamoja, na kunufaika na fursa zinazotokana na ushirikiano kwenye "ukanda mmoja, njia moja".

    Tanzania pia inashiriki kwenye mkutano huo kama mwalikwa maalum, na naibu waziri mkuu Bw Han amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Tanzania Balozi Seif Ali Iddi. Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi anasema

    "Nawashukuru waandaaji wa mkutano huo kwa kuichagua Tanzania, kuwa mshiriki maalum kwenye mkutano huu wa 15 kati ya China na nchi za ASEAN. Kwetu sisi hii ni heshima kubwa, na ni ushahidi wazi wa kuwepo kwa urafiki na ushirikiano wa kimkakati usiotetereka kati ya China na Tanzania…. Tanzania na nchi za ASEAN, hasa China, zimekuwa zikinufaika sana kutokana na kushirikiana kwa miaka mingi, na kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi, na inafurahisha kutaja kuwa ushirikiano wetu wa karibu umeimarisha ushirikiano kati ya watu na watu kwenye mambo ya biashara na utamaduni, wafanyabiashara wa China sasa wamezoeleka nchini Tanzania na wafanyabiashara wetu wanakuja sana China"

    Mbali na mkutano kati ya viongozi wa nchini zinazoshiriki, maonyesho ya biashara yanafanyika sambamba na mkutano huo. Tanzania ambayo ni ni nchi ya kwanza ya Afrika kualikwa kwenye maonyesho hayo, ina mabanda yapatayo ishirini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako