• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Startimes iko tayari kurudisha chaneli za bure

    (GMT+08:00) 2018-09-12 18:51:08

    Kampuni ya Star Media Tanzania limited inayomiliki kisimbuzi cha Startimes, imesema tayari imerudisha chaneli za bure (FTA) katika visimbuzi vyake (bila kutaja idadi) ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

    Julai 27, TCRA ilitoa tangazo kwa umma likielezea nia yao ya kuzuia leseni ya kampuni hiyo kwa madai kuwa ilikiuka masharti yake. Miongoni mwa masharti hayo ni suala la kutoonyesha FTA na kutolipa faini iliyotozwa jambo ambalo ni kinyume na masharti ya leseni yake.

    Tangazo la TCRA ambalo lilionekana kusainiwa na mkurugenzi wake mkuu, James Kilaba lilieleza kuwa hata baada ya Startimes kutakiwa kurejesha huduma ya bure kwa baadhi ya chaneli hawakufanya hivyo badala yake wananchi waliendelea kulalamika.

    Akizungumza na radio China kimataifa, msemaji wa Startimes Juma Suluhu alisema tayari wamerudisha chaneli za bure katika visimbuzi vya wateja wao tangu mamlaka ilipowataka kufanya hivyo. Awali, Startimes ambayo ndiyo kampuni inayoongoza kwa wateja wengi kati ya zote zenye leseni ya kurusha FTA ilitoa mwongozo kuhusu namna ambavyo wateja wake wanaweza kupata chaneli hizo.

    Mwongozo huo ulisema kampuni hiyo ina visimbuzi vya aina mbili, kimoja kinaonyesha chaneli za bure kuanzia 6 hadi 16 kutokana na mahali alipo mteja wa FTA na bei yake ni Sh89,000 na kingine chaneli hizo huonekana baada ya kulipia (Pay TV Decoder) ambayo ni Sh45,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako