• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kujenga mustakabali mzuri wa Mashariki ya Mbali na Asia Kaskazini Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-09-12 19:07:28

    Mkutano wa 4 wa Baraza la uchumi la mashariki umefanyika leo mjini Vladivostok, Russia, na kuhudhuriwa na rais Vladmir Putin wa Russia, rais Xi Jinping wa China, na rais Khaltmaa Battulga wa Mongolia, pamoja na waziri wakuu wa Japan Shinzo Abe na waziri mkuu wa Korea Kusini Lee Nak-yon.

    Katika mkutano huo, Rais Xi amesisitiza kuwa, kuijenga Asia Kaskazini Mashariki iwe ya masikilizano, kuaminiana, mshikamano na utulivu kunalingana na maslahi ya nchi mbalimbali na matarajio ya jumuiya ya kimataifa. Anasema:

    "China siku zote inashikilia wazo la kujiendeleza kwa amani, imekuwa ikifanya juhudi za kujenga mazingira yenye ujirani mwema na kirafiki, kufanya ushirikiano wa kikanda kutokana na mtizamo wa kiujenzi, na kuhimiza nchi mbalimbali za kanda hiyo kufanya mawasiliano na mazungumzo. China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kutafuta njia yenye ufanisi ya kulinda amani na usalama wa kudumu kwenye kanda hiyo, na kufanya juhudi bila ya kusita katika kutimiza amani, utulivu na maendeleo kwenye kanda hiyo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako