• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China imekuwa msukumo mpya katika kuhimiza ujenzi wa umoja wa uchumi wa Asia Kaskazini Mashariki

  (GMT+08:00) 2018-09-12 21:01:09

  Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba katika mkutano wa Baraza la 4 la uchumi la Mashariki uliofanyika mjini Vladivostok, Russia.

  Hotuba hiyo ilihusu kunufaika kwa pamoja kutoka kwa fursa mpya za maendeleo ya Mashariki ya Mbali na kuunda mustakabali mpya ya Asia Kaskazini na Mashariki. Rais Xi ametoa maoni manne ya kuhimiza amani na utulivu na ufanisi wa maendeleo wa kanda hilo chini ya hali mpya, ambayo ni kuhimiza kuaminiana, kuimarisha ushirikiano, kujifunza kutoka kwa kila mmoja, na kuona kwa umbali. Hotuba hiyo imeunda mipango na kuingiza nguvu mpya kwa kujenga maeneo ya uchumi ya Asia Kaskazini na Mashariki, kuhimiza sekta mbalimbali za kanda hiyo na maendeleo endelevu.

  Rais Xi Jinping ameweka lengo la pamoja la kuanzisha Maingiliano ya Kiuchumi kwa nchi za Asia Kaskazini Mashariki, ambalo lina msingi thabiti. Kwanza sehemu ya Asia Kaskazini Mashariki ina raslimali kubwa ya asili, pili, sehemu hiyo ina uwezo mkubwa wa kuongoza nchi nyingine duniani katika kufanya utafiti wa sayansi, China, Russia, Japan na Korea Kusini zote ni nchi zenye nguvu za sayansi na teknolojia. Mbali na hayo, sehemu hiyo ina fedha za kutosha, hususan uwekezaji wa China katika nchi za nje umekuwa msukumo muhimu katika kuhimiza ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja duniani, na hali ya usalama inayozidi kuboreshwa katika sehemu hiyo pia imehakikisha vizuri ushirikiano wa kikanda.

  Je, jinsi gani pande mbalimbali zitakuza ushirikiano kati yao zikikabiliana na hali mpya? Rais Xi ametoa mapendekezo mbalimbali yakiwemo "kuoanisha mikakati ya maendeleo", "Kuinua kiwango cha uunganishaji wa miundo mbinu kwa kuvuka mipaka ya nchi, na biashara na uwekezaji huria".

  Hivi sasa, pendekezo lililotolewa na China kuhusu ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja limekaribishwa na nchi za Asia Kaskazini Mashariki, ambazo zimeeleza matumaini ya kuunga mkono na kushiriki kwenye ujenzi huo. Rais Xi amesema, China na Russia zinafanya juhudi kuunganisha ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na Umoja wa uchumi wa Ulaya na Asia, pia zimepata mafanikio muhimu ya mwanzo.

  Kwa upande wa muda mrefu, mzunguko wa uchumi wa Asia Kaskazini Mashariki unaofunguka si kama tu utaleta faida kwa watu wa kanda hiyo, bali pia utakuwa nguvu muhimu ya kulinda siasa za pande nyingi, na kuhimiza utaratibu wa kimataifa uelekee kwa mwelekeo wa haki zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako