• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Russia watumaini vijana wa nchi hizo mbili wataenzi urafiki kizazi baada ya kizazi

  (GMT+08:00) 2018-09-13 18:27:19

  Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Vladimir Putin wa Russia jana kabla ya kurejea Beijing walitembelea Kituo cha watoto wa Russia cha "Bahari" huko Vladivostok, Russia. Viongozi hao wawili wana matumaini kuwa vijana wa nchi hizo mbili wataimarisha mawasiliano, na kuenzi urafiki kati ya pande hizo mbili kizazi baada ya kizazi.

  China na Russia ni majirani wema na marafiki wazuri, na watu wa nchi hizo mbili wamekuwa wakikabiliana kwa pamoja matatizo mbalimbali. Kituo cha watoto cha "Bahari" cha Russia kilichoko huko Vladivostok kimeshuhudia urafiki huo mkubwa kati ya watu wa pande hizo mbili.

  Kabla ya kufunga safari ya kurudi nchini China kutoka Russia jana usiku, rais Xi akiongozana na rais Putin alihutubia sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kituo cha watoto cha "Bahari" cha Russia kiwapokee watoto wa China walioathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea huko Wenchuan, China, mwaka 2018. Rais Xi anasema:

  "Baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea huko Wenchuan, China, mwaka 2008, kikosi cha uokoaji cha Russia kilifika eneo la maafa mapema na kutoa msaada bila hiyana. Kutokana na mwaliko wa serikali ya Russia, wanafunzi 996 wa shule za sekondari na za msingi walioathirika na maafa hayo, walipelekwa kwenye kituo hicho cha watoto nchini Russia na kutunzwa kwa makini. Kwenye bahari hiyo yenye upendo, watoto walifarijika huku upeo wao wa macho ukipanuka, na pia wamepata urafiki wa dhati."

  Rais Xi ameeleza kuwa historia ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia vilevile ni historia ya mawasiliano ya karibu kati ya vijana wa pande hizo mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, mawasiliano yanayofanyika mara kwa mara kati ya vijana wa nchi hizo mbili yameongeza uelewa na urafiki kati yao. Rais Xi pia amesisitiza kuwa, vijana ni mustakabali wa nchi hizo mbili, mustakabali wa urafiki kati ya pande hizo mbili, pia ni mustakabali wa dunia. Rais Xi anasema:

  "Natumai kuwa vijana wa nchi hizo mbili watathamini wakati, kujifunza kwa bidii na kutoa mchango mapema kwa ajili ya nchi zao; kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na kuenzi urafiki kati ya China na Russia kizazi baada ya kizazi; kujitahidi kushiriki katika mazungumzo kati ya ustaarabu tofauti, ili kujihusisha katika kazi ya kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja kwa busara na nguvu zao. Pia nikiwakilisha serikali na watu wa China, nawaalika mje China na kufurahia ukarimu mkubwa wa wananchi wa China."

  Naye rais Putin ameeleza kuwa, Russia na China zimeunda uhusiano wa kirafiki wa kuaminiana na kushirikiana. Mawasiliano ya kirafiki kati ya vijana wa nchi hizo mbili yatawekea msingi imara kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambayo yatakuwa na umuhimu mkubwa kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili katika siku za baadaye. Natumai kuwa vijana wa Russia na China wataenzi urafiki mkubwa wa jadi kati ya pande hizo mbili kizazi baada ya kizazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako