• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za ASEAN wasifu Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China

    (GMT+08:00) 2018-09-13 19:46:49

    Maonesho ya 15 kati ya China na nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN, ambayo pia ni Mkutano wa kilele wa biashara na uwekezaji kati ya China na ASEAN umefunguliwa jana mjini Nanning, mkoani Guangxi, China. Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo, viongozi mbalimbali wa nchi za ASEAN wamesifu pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", pamoja na maonesho hayo.

    Akihutubia ufunguzi wa maonesho hayo, Naibu waziri mkuu wa Laos amesema pendekezo hilo lina umuhimu mkubwa katika kuendeleza uhusiano wa biashara kati ya China na ASEAN, hususan miradi muhimu inayohusu pendekezo hilo. Nchi mbalimbali za ASEAN zinapaswa kuchukua fursa nzuri zinazoletwa na eneo la biashara huria kati ya China na ASEAN, kuimarisha ushirikiano na kutoa fursa mpya kwa biashara na uwekezaji kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako