• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushuru wa VAT kufanyiwa kufanyiwa marekebisho

  (GMT+08:00) 2018-09-14 19:11:44

  Ushuru wa zaidi ya thamani (VAT) unaofikia asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta utafanyiwa marekebisho 'siku chache zijazo' baada ya kusikika kilio cha wananchi tangu ulipoanza kutekelezwa Septemba 1, 2018, na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta na vilevile mfumkobei kwa jumla.Waziri wa Fedha Henry Rotich amesema Alhamisi kwamba wizara yake iko katika hatua za mwisho za kuafikiana na Bunge kuhusu suala hilo baada ya msururu wa mazungumzo yaliyoanza wiki jana.

  Hii ni baada bunge la kitaifa kuufanyia marekebisho Mswada wa Fedha ambao uliahirisha utekelezaji wa ushuru huo kwa muda wa miaka miwili. Ameongeza kuwa alihudhuria mazungumzo kuhusu suala hilo katika kikao kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi, kauli ambayo pia ilitolewa na waziri msaidizi wa fedha Nelson Gaichuhie alipofika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Kawi.Rais ameurejesha mswada huo bungeni na taarifa akitaka ufanyiwe mabadiliko ili kurejesha kipengee kinachoruhusu utekelezaji wa ushuru huo wa ziada ya thamani (VAT).

  Hatua ya Rais inajiri saa chache baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kuwasilisha mswada huo kwake ili aushughulikie. Ushuru huo umesababisha gharama ya maisha kuongezeka ikiwamo nauli, bei ya sukari na unga. Bw Kenyatta Alhamisi licha ya kuhutubu kwa mara ya kwanza tangu arejee nchini, ameonekana kusalia kimya kwa ushuru huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako