• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyuo vikuu vinavyowapendeza waajiri zaidi Afrika

  (GMT+08:00) 2018-09-14 19:12:48

  Ni shahada ya chuo kikuu gani Afrika ambayo inapendelewa na waajiri zaidi duniani? Afrika Mashariki kuna chuo kikuu kimoja pekee, vyuo vikuu vingine vikitoka Afrika Kusini na Misri.

  Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa 'Kuajirika kwa Wanaofuzu na Shahada Duniani wa 2019' ambao umefanywa na kampuni ya QS Group na huwa kiashiria cha matumaini ambayo wanafunzi wanaweza kuwa nayo wakitafuta kazi baada ya kufuzu.

  Aidha, huwa ni kiashiria kwa vyuo vikuu kwamba vinafaa kujivunia kazi na juhudi zao.

  Kampuni ya QS Group pia hutayarisha Orodha ya Vyuo Vikuu Bora Duniani.Orodha ya sasa imetayarishwa baada ya kutafuta maoni ya waajiri 42,000 kote duniani na ni kiashiria cha chuo kikuu gani kinapendwa zaidi na waajiri.

  Waajiri waliulizwa kuhusu ni wapi watu wenye shahada walio na "ujuzi zaidi, ubunifu na uvumbuzi na wanaomudu kazi vyema zaidi" hutoka. Chuo hicho kikuu cha Nairobi ndicho pekee kutoka Afrika Mashariki ingawa kimeshuka kutoka nambari tano Afrika mwaka 2018, mwaka ambao kulikuwa na vyuo vikuu 11 vya Afrika katika vyuo vikuu 500 bora duniani kwenye orodha hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako