• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi Seif asifu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa Tanzania na China

  (GMT+08:00) 2018-09-14 19:24:00

  Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Tanzania Balozi Seif Ali Iddi amesema, biashara kati ya Tanzania na China inaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, hali ambayo inasaidia kuongeza mapato ya Watanzania na kuboresha maisha yao. Alisema hayo jana alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kwenye ufunguzi wa onyesho la bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya 15 ya China na Umoja wa nchi za Asia Kusini Mashariki ambayo yanafanyika mkoani Guangxi, kusini mwa China. Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na balozi Seif unashiriki kwenye maonyesho hayo ya bidhaa.

  Balozi Seif alisema, China inaagiza mihogo mingi kutoka Tanzania. Muhogo ni mazao kuu nchini Tanzania. Kila mwaka China inaagiza toni elfu 60 ya mihogo, lakini bado kuna upungufu mkubwa. Hivi sasa serikali ya Tanzania inawahimiza wakulima kupanda mihogo zaidi, ili kuuza mihogo mingi zaidi kwa China, na kuongeza mapato ya wakulima wake. Ameongeza kuwa China ni soko bora zaidi la mazao ya Tanzania.

  Tanzania ikiwa ni nchi muhimu barani Afrika kwenye njia ya hariri baharini, imealikwa kushiriki kwenye maonyesho hayo yanayofanyika Jumatano hadi Jumamosi wiki hii nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako