• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Yemen yaimarisha uwepo wake kijeshi kwenye mji wa Hodeidah

    (GMT+08:00) 2018-09-17 09:30:14

    Serikali ya Yemen imeimarisha uwepo wake katika mji wa Hodeidah ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya hatua kubwa zaidi dhidi ya waasi wa Houthi katika mji huo.

    Zana nzito kwa ajili ya brigedi ya kusini zimeendelea kupelekwa Hodeidah, wakati jeshi la serikali linaloungwa mkono na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, likiwa linajiandaa kuwafukuza wapiganaji wa Houthi kutoka mji wa Hodeidah.

    Vikosi vya serikali pia vimewasili kutoka Aden na kwenye majimbo mengine yanayodhibitiwa na vikosi vya serikali, vikiwa tayari kufanya shambulizi la kuukomboa mji wa Hodeidah na jimbo zima.

    Wakati huo huo habari zinasema waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wanaimarisha vikosi vyao, kujiandaa na mapambano dhidi ya vikosi vya serikali ya Yemen, vinavyoungwa mkono na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, ambayo imewapatia wapiganaji wa serikali mamia ya maderaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako