• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia mkutano kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini kupata matokeo mazuri

    (GMT+08:00) 2018-09-17 18:48:32

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inatarajia mkutano kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini utapata matokeo mazuri.

    Amesema China itaendelea kuunga mkono pande mbili za peninsula ya Korea kuboresha uhusiano wao, kuendelea kufanya juhudi na kutoa mchango kwa ajili ya kutimiza peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia na usalama wa kudumu wa Asia ya Kaskazini Mashariki.

    Bw. Geng Shuang amesema, China inatumai mkutano huo utaimarisha utaratibu na mawasiliano kati ya pande mbili, kuongeza na kuimarisha mwelekeo wa kupunguza mvutano katika peninsula ya Koera, na kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa suala la peninsula ya Korea kwa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako