• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya: Msimu mpya kuanza leo

    (GMT+08:00) 2018-09-18 09:26:28

    Msimu mpya wa ligi ya klabu bingwa ulaya wa mwaka 2018-2019 unaanza rasmi usiku wa leo ambapo jumla ya mechi nane kati ya timu kutoka makundi A, B, C na D zitashindana katika michezo ya mzunguko wa kwanza.

    Miongoni mwa mechi zitakazopigwa kesho, PSG ya Ufaransa itakuwa na kibarua kizito ugenini dhidi ya Liverpool ya Uingereza, nayo Inter Milan itakuwa nyumbani nchini Italia kuikatibisha Tottenham ya Uingereza.

    Barcelona ya Hisapania itakuwa nyumbani kucheza na PSV ya Uholanzi, Monaco ya Ufaranza ikicheza na Atletico Madrid ya Hispania.

    Nayo Crvena Zvezda ya Serbia itacheza dhidi ya Napoli ya Italia, Schalke ya Ujerumani dhidi ya Porto ya Ureno, Lokomotiv Moscow ya Urusi itakuwa ugenini nchini Uturuki kucheza na Galatasaray, na Club Brugge ya Ubeligiji itaikaribisha Borussia Dortmund ya Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako