• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaimu mkuu asema IAEA inashirikiana vizuri na China

    (GMT+08:00) 2018-09-18 10:06:34

    Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani IAEA Bibi Alice Hayward amesema, shirika hilo lina ushirikiano mzuri na China, na utaalamu wa nishati ya nyuklia wa China unazifaidisha nchi nyingine wanachama wa shirika hilo.

    Mkurugenzi wa Shirika la Nishati ya Atomiki la China Bw. Zhang Kejian amejulisha mkakati wa China katika matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia, akisisitiza kuwa China itashikilia maendeleo yenye masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili, kurekebisha na kuboresha muundo wa nishati. Amesema nishati ya nyuklia ikiwa nishati safi ambayo inatoa kiasi kidogo cha kaboni, itapata maendeleo katika maeneo mapya.

    Mwezi Mei mwaka 2012, kampuni ya uranium ya China CGNPC, ikishirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya China na Afrika ilifanikiwa kununua Madini ya Uranium ya Husab nchini Namibia. Miaka minne na nusu baada ya kujengwa kwa kiwanda, pipa la kwanza la uranium ghafi lilizalishwa, na uzalishaji wa mwaka jana ulifikia tani 1,345. Mradi huo umetimiza lengo la ushirikiano wa kuleta manufaa kwa pande mbili katika jangwa la Namib kutokana na sio tu kuipatia Namibia injini mpya ya maendeleo yasiyochafua mazingira na faida kwa watu wa Namibia na pia kutoa nishati kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa nyuklia ya China, na kuongeza imani ya maendeleo yenye ufanisi na usalama ya umeme wa nyuklia nchini China, na kuonyesha moyo wa ushirikiano wa kunufaishana wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako